A Grain Of Wheat Ministries

Kosa La Uandishi

Kosa La Uandishi by David W. Dyer

Martin Luther alipotundika mapendekezo yake 95 katika lango la jengo la kanisa la Kiroma, Ulikuwa tu ndio mwanzo wa yale ambayo leo tunayaita “Mageuzi”. Alichotaka zaidi ulikuwa kuonyesha makosa ya Kanisa na kulirudisha kanisa lenyewe kwake Mungu. Lakini aliyoyaona na kuyaandika hayakuwa kwa njia yoyote halisi na ya kueleza kwa kikamilifu jinsi Kanisa la Kiroma liliepuka ukweli. Katika enzi hizo, ufunuo wa kiroho ulikuwa umepotea. Mambo mengi ya kihalisi ambayo hayazingatiwi kwa kina katika kizazi chetu (kama vile wokovu kwa imani) hayakuwa yamebainika. Hivyo basi Mungu alimtumia huyu ndugu kwa uwezo wake ili kutueleza haya tusiyoyajua na pia kutambua kitu tofauti. Miongo ilivyopita, Mungu amezidi kutumia watumishi wake ili kuuleta upya ufunuo katika mwili wake. Mambo kama matumizi yakiwapo na kazi za karama za roho mtakatifu, ibada za kikweli za kiroho, ubatizo - kwa kutaja tu chache - kwa sasa yamechukuliwa mara nyingi kanisani kuwa mambo ya kawaida. Tangia wakati wa Luther, kumekuwapo na kukua kukiandamana na ufunuo wa ukweli wa Mungu kwa watu wake.

Mtindo huo haujakoma, sisi kama kanisa hatujawasili na hatutawasili hadi kurudi kwake Kristo na utukufu wake. Kwa hivyo tukitamani kupewa kipaumbele katika matendo ya Mungu, ni lazima tuwe tayari kupokea na kutenda kwa njia anayotuonyesha katika wakati huu. Yanayofuata ni baadhi ya yale ambayo ninaamini Mungu angependa kuleta upya katika siku hizi. siyo yale tunayoyadhania kuwa mapya tu, wala sio ufunuo wangu wa kibinafsi. Haya ni mambo ambayo wakristo wengi wa kweli wameelewa katika muda usiopungua mwongo mmoja. Ingawa, mienendo ya kawaida ya mwenye dhambi hufanya ukweli huu kuwa mgumu kutekeleza na kulinda.

Kuanzia jadi, aliyoyapenda Mungu kwa mwanadamu hayajabadilika, angependa kutembea nasi kila mara na kushinda nasi katika ibada. Hii ndiyo sababu yake kuu ya kumwumba Adamu, nia yake katika kuwaita wana wa Israeli kwake na pia nia yake kwa kanisa la leo. Nia hii ya upendo wake siyo tu kwa ujumla wa watu wake bali pia ni kwa kila mmoja wetu kibinafsi. Ari kuu yake Mungu ni kustawisha mapenzi katika uhusiano wake nasi na ndio utakaobadilisha tabia na maumbile yetu ili yawe kama yake.

Mwanzoni Mungu alijihusisha na watu binafsi kama vile Nuhu, Seth na Enoka. Baadaye tunaonyeshwa jambo la “watu wa Mungu” tunaposoma kumhusu Musa na wana wa Israeli jangwani. Lakini hapa pia Mungu hakupendelea tu ule uhusiano wa kijumla na wale waliofwatilia dini, bali alipendelea kuwa na uhusiano wa kipekee, wenye mapenzi ya dhati na kila mmoja wao.

Mapema kidogo, katika kipindi cha miezi mitatu bada yao kutoka Misri, Mungu alinena naye Musa kuwahusu Waisraeli. Hapa alionyesha nia yake halisi na ya juu zaidi kwao. Alisema : watakuwa “Kwangu Ufalme wa makuhani” (Kutoka 19:6). Maelezo haya yanatueleza aina ya uhusiano alioupenda Mungu akiwa nao na kila mmoja wao. Alionyesha mapenzi ya dhati ambayo yangewawezesha kusimama mbele mbele zake na kufanya kazi zao za kikuhani. Katika enzi hizo haya yangehusisha kazi kama kumhubiria Mungu katika ibada na maombi kwanza, kisha kilichotokana na uwepo wa Mungu kingehubiriwa wengine. Haukuwa mpango wake Mungu kuwa watu wajue tu kumhusu kisha baadaye kuzama katika vipindi vya mafundisho ya kidini. Mungu wetu alitaka sana watu wamtambue na wahusiane naye kwa kipekee na kwa mapenzi ya dhati.

Lakini mjuavyo, wana wa Israeli hawakuwa na uhusiano huu naye Mungu. Alipoanza kujongea karibu nao na kuonysha utakatifu wake kwenye mlima Sinai, walimwepuka Mungu na kumsukuma Musa mbele wakisema “zungumza nasi na tutasikia lakini usimwache Mungu anene nasi, tunaweza kufa” (Kutoka 20:19). “Kwa hivyo watu walisimama mbali, lakini Musa alisongea karibu na lile giza kuu ambalo Mungu alikuwapo” (Kutoka 20:21). Mioyo yao haikuwa sawia na yake Mungu kwa hivyo alipoanza kuzungumza nao hakuweza kutafakari. Katika muda uo huo waliukwepa mwito wa juu ambao Mungu aliwapa na walimwacha mtu mwingine kuhusiana na Mungu badala yao. Badala ya kuomba msamaha baada ya kuyasikia maneno yaliyoeleza utakatifu wa Mungu na kumwacha awasafishe upya, walichagua kurefusha hatua kati yao na Mungu na kumleta mpatanishi kati yao na Mungu ambaye angechukulia majukumu yao.

Huku kuepukana na ukweli wa Mungu uliwazalia matunda baadaye. Musa alipochukua muda katika uwepo wa Mungu, wao walipendezwa na tamaa zao. Uhusiano wao wa kibinafsi na Mungu muumba wao ulididimia kiasi yao kushuku hata kuwepo kwa Mungu na uwezo wake kusalimisha ahadi zake kwao. Suluhisho lao likawa kujiumbia mungu ambaye hakuwa na utu wala utakatifu na pia aliyekuwa rahisi kurai – yule ambaye hangewatisha na ambaye uwepo wake haukuwa na mahitaji ambayo wao wenyewe hawangeweza kutimiza. Wakati huu Mungu alikuwa ameshaamua kuwatupilia mbali na wakawa hawatoshi kiwango cha kuwawezesha kuhitimu na kutenda nia awali ya Mungu (Kutoka 32: 9, 10).

Pengine ni kwa vile mioyo ya watu kwu jumla hayakumwitikia Mungu ndiposa aliteua kikundi muhimu cha makuhani. Yaweza kuwa ni kabila la Lawi ndilo liliteuliwa kwa vile walikuwa na ari ya kumsikiza Mungu, angalau kwa kipimo fulani, na kutimiza maamuzi yake Mungu (Kutoka 32:28). Kwa hivyo tunauona uchaguzi wa kikundi cha ukuhani kitakachokuwa karibu na Mungu kwa hisani ya watu kwani ushirika wa kijumla ulipoteza mapendeleo ya kuwa yote ambayo muumba wao aliwataka kuwa. Ukuhani wa kilawi ulikuwa kwao kama kizuizi au eneo la bainifu ambao ulimfanya Mungu kuonekana kuwa mbali nao na kuwafanya kujihisi kuwa na starehe.

Tunapata picha sawia na hii tunaposoma kitabu cha Samweli wa kwanza. Wakati huo wana wa Israeli hawakuwa na mfalme. Alichotaka Mungu ni kuwa wangekuwa watu wa kipekee kati ya watu wote wa ulimwengu – watu waliotawaliwa kwa kipekee na Mungu wao mwenye nguvu asiyeonekana. Ingawa, watu walilitupilia jambo hili. Kukamilisha mpangilio huu ilibidi wastawishe uhusiano wao na Mungu, wakijifundisha kumwamini na kumfwata. Jambo hili halikuwa rahisi, hasa kwa mtu wa kawaida. Kwa hivyo watu hawa walitupilia tena mpango wa Mungu wakasisitiza kuwapo kwa mfalme wa kidunia. Walitamani kuwa na mfalme kamili, binadamu ambaye wangemwona mtu ambaye angechukua hakimu za uongozi kwao, mtu ambaye angesimama kati yao na Mungu. Samweli kwa hakika hakukubaliana na pendekezo hili, lakini Mungu alimtulizisha kwa kumwambia, “hawajakutenga, lakini wamenitenga ili nisiwatawale” (1 Samweli 8:7).

Kutokana na hili tunaelekezwa katika hali yetu ya leo. Si jambo la kushangaza kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya wakristo wa sasa nao watu wa Mungu wa Agano la kale. Historia ya kanisa yatueleza kuwa si kitambo sana baada ya kutoka kwa mitume wa awali, Viongozi wa kanisa walianza kupata sifa za kuzidi mara kwa mara. Maaskofu walianza kuzidisha uwezo wao kwa zaidi ya jiji moja na hatimaye kwa maeneo kamilifu. Nafasi za kidini zilisisitizwa zaidi na umuhimu wa kujitolea katika nafasi hizi. Mbinu hii imeenea katika miongo, hadi kufikia kukomaa katika ukatoliki wa Kiroma. Baadaye maandishi yalitolewa katika mikono ya watu, kisha huu mtindo wa “mpatanishi” ambao tumeshinda tukieleza ulipata kukomaa. Hatufai kushangazwa na mwenendo kama huo. Ni jambo la kawaida na pia la kibinadamu. Kwa hakika, bila majaribio ya kinyume kufanywa, mashirika yote ya kikristo yanaonekana kuwa yatazembea katika mwenendo huu.

Leo hii, ingawaje Uprotestani umefanya maendeleo dhidi ya tatizo hili kukiwapo giza na kuabudu miungu inayopatikana katika mtindo wa kiroma, bado umehifadhi baadhi ya makosa haya. Ilhali maandishi yanafundisha kuhusu uchungaji kwa waumini wote (1 Pet. 2:5,9), mbinu za baadhi ya makanisa ya kikristo zinaupinga. Baadhi ya tunayoyaona katika makanisa ya leo ni utumishi wa mmoja au wateule wachache, wengi waliosalia wakiwa ni watazamaji tu, wasiofanya lolote. (Jer. 5:31). Ninahakika kuwa hoja hii haihitaji maelezo yoyote ya kina bali inafaa kuonekana wazi kwa hata mtazamaji asiyezingatia mengi. Bila shaka, maelezo haya yakiwa hayawiani na unayoona katika kanisa lako, ninafurahia nawe katika matumaini kuwa unasherekea matunda yake.

Kwa kweli uongozi wa kisasa kati ya mashirika ya kikristo halijatambuliwa kuwa “uchungaji.” Hilo litakuwa lisilotambuliwa katika maandishi kwa wazi. Badala yake tunavyo vitambulisho kama vile “ Mchungaji,” “Mhudumu” , au “Mtume.” Lakini kazi za hawa watu ni kwa hakika sambamba na kazi za kuhani wa agano la kale. Ndio “wanaopata ujumbe kutoka kwa Mungu,” wanaofanya mafundisho, kupatiana maelezo, kupangilia na kadhalika. Inasemekana na pia ni kweli kuwa katika hali nyingi “mchungaji” anatakikana kufanya kadri kila kitu.

Kwa vile huu ni mwenendo uliokita kati ya waumini wa leo na unaonekana kutambuliwa katika ulimwengu mzima, wengi wanaweza kujiuliza ni nini mbaya nao. Huu ni mtazamo muhimu. Ili kuelewa jawabu lake, ninaamini kuwa ni lazima tuhusishwe kwa uhakika katika nia na mapenzi ya Mungu. Binadamu angekuwa mhusika pekee katika hali hii labda maelezo yetu hayangekuwa ya kutiliwa maanani vilivyo. Lakini hapa tunajaribu kuelewa na kutimiza mahitaji ya Mungu hivyo basi tunapaswa kuzingatia hoja yetu kwa heshima na hofu. Si hivi tu bali tunapaswa kuelewa kuwa nia yake kuu ni kwa wema wetu na mapendeleo yetu. Bila shaka tunavyozidi kuviona vitendo vya Mungu tutagundua kuwa maelekezo na mahitaji yake siyo tu yake kujivunia bali ni kwa kutustawisha milele.

Mpango wa Mungu kwa kanisa ni mara dufu. Kwanza, ametueleza tuipeleke injili yake katika kila pembe ya duna. Pili, anatarajia kuwa tutabadilishwa katika umbo lake. Sasa tukiwa tutauchukua ujumbe huu kwa nguvu na uhakika wote ili kutimiza mwisho huu, inatupasa kuwa watu walio karibu na Mungu! Kila mmoja wetu lazima awe katika uhusiano wa kipekee na muumba wetu na kuutunza uhusiano huu. Sote tunatakikana tuwe wachungaji. Kisha baadaye kutokana na uhusiano huu, tuzalishe huduma ya uchungaji ambayo itakamilisha mpango wa Mungu.

Hatufai kuwatazamia viongozi au wenye vipawa kuhakikisha kuwa jambo limefanywa. Hatufai kutegemea mashirika ya kimataifa na shinikizo za kila mara. Kila mmoja wetu anapaswa kubeba kiasi fulani cha jukumu hili. Ukweli ni kuwa, bila ya kuhusika katika kuwahubiria wengine, iwe ni katika mahubiri ya injili au kwa kuhusisha vipaji vyetu vya kiroho, basi tumeingia katika kosa. Mungu anataka kila mmoja wa watu wake aajiriwe katika kazi yake. Sote tu watumishi na tumeitwa na kuchaguliwa na Mungu kufanya kazi ya huduma ya uchungaji hadi atakaporudi (Yohana 15: 16).

Yesu Kristo alipopaa kwa baba yake alituachia vipaji katika kanisa lake. Hivi “vipaji” au karama za kiroho hazikupewa wachache walioteuliwa bali wote (1 Wakorintho 12: 7). Kila sehemu inayo kazi yake yenye manufaa, jinsi vilivyo viungo na kila sehemu ya mwili wetu. Hata ikiwa kiungo au sehemu ionekanayo kutokuwa na maana haifanyi kazi yake vyema, mwili wote huugua. Hii pia ni kweli katika kanisa la leo. Wakati mtu mwenye kipaji fulani maalum au mwenye “somo” fulani anapofanya kazi zote kunao uhaba katika mwili wa Kristo na pia kwa Mungu.

Kweli ninaomba kuwa kila anayesoma haya maandishi atauchukua ukweli huu moyoni mwake. Haijalishi unachofikiria kujihusu au kuhusu uwezo wako wa Kiroho. Wala si ya maana unavyojilinganisha na watu wengine. Hata wale wenye kipaji kidogo wanatakikana na watatakikana na Mungu kukitumia kwa kikamilifu. (Mathayo 25: 14-30).Tukihadaiwa kwa kujilinganisha na watu wengine au kuogopa na kutofanya lolote tutamjibu Muumba siku moja. Ni haki na jukumu letu la kupendeza mbele za Mungu kugundua kazi aliyotuita tufanye na tuanze kujifundisha kwa Roho yake Mungu, tujifanyie majaribio tukielekea mwisho huu.

Bila huduma kama hii, hatutaweza kukua kikamilifu . Lau, tungeuchukua mtindo wa kiroho -hasa mwanzoni– lakini, kukua hadi kukomaa ni lazima tuanze kwa kujihubiria. Tunavyopeana ndipo tunapewa mengi. Hii ni sheria ya kiroho. Tukiwa wa kupokea tu - baada ya kila juma tukiskiza mafundisho ya wale waliochukua muda wao katika uwepo wa Mungu - ujuzi wetu utakua lakini maisha yetu hayatabadilika. Hili ni jambo la kuhuzunisha katika wingi wa kanisa la leo. Tumekuwa “washindi” wetu kibinafsi ambao labda tumejulikana, na tunashughulika usiku na mchana, lakini pia tunao “wazembe wengi” wanaotegemea wengine kuwafanyia kazi zao.

Sababu haribifu katika hali hii haiwezi kuonekana kwa wazi, hasa katika shirika lilokomaa, lakini hazisaidii kikamilifu. Mikutano mingi ya kikristo imejazwa na watoto wa kiroho ambao wameshibishwa lakini kufanyishwa kazi kidogo. Wao huja kila juma na kudhani kuwa kwa vile wanasikia mafundisho mazuri basi wako inavyopasa na Mungu. Lakini kila mara watu hawa huwa na dhambi zilizofichwa au makosa mazito katika nafsi zao. Ni kila mara tunapowahudumia wengine ndipo dhambi hizi hufichuliwa. Tunapoanza kuhudumu tunagundua kuwa maisha yetu yanahitaji kubadilika na hili llinatupa sababu za kumtafuta Mungu ili tupate ukombozi. Tukielekea katika kukomaa kiroho kwa ukweli, inatubidi kuwa wachungaji – wachungaji ambao wanajihusisha kwa kweli katika kazi zao katika nyumba ya Mungu.

Sizo tu huduma za kiroho ndizo zinatubidi kukua, la maana pia ni mwenendo wa wengine. Bila ya kushughulika na uwezo wako wa kiroho au kazi za mwili wako, kunao wengine wanaohitaji ulicho nacho. Haijalishi kama chako ni kidogo au kikubwa. Bila shaka kinahitajika pahali fulani kati ya waumini unaowajua au ulimwenguni kunao wale ambao sehemu yako ina maana kwao. Kwa mfano majirani wako wanaweza kuwa wanaangamia bila ya Kristo kwa sababu ya woga wako au wewe kutotaka kuwaongelesha. Labda marafiki wako wakristo wanaweza kuwa wanatafuta lile ambalo unajua. Yawezekana kuwa wengi wa unaowajua wanateseka kwa sababu hujachukua muda kuombea ukombozi wao au kutilia maanani mahitaji yao. (Ni rahisi mno kukashifu au kusengenya kushinda kuombea au kusaidia, sivyo?)

Waona, sehemu yako ni ya maana katika kukua, na kustawi kiroho kwa wengine. Mungu amekupa sehemu hii kwa hisani yao kwa hivyo ni jambo la maana kuitumia. Kwa hekima yake, Baba yetu amejenga kanisa ili kila mshiriki awategemee wengine. Kwa hivyo, “ uhakikisho wa wote” katika kukomaa (Waefeso 4: 13), huduma za kila sehemu ni za muhimu.

Wakati huu wengine wanaweza kujiuliza, “Viongozi wa kidini wanafaa wapi katika haya yote?” uongozi upo katika maandishi na pia unahitajika katika hali ya kanisa lenye afya. Ingawaje huwa haieleweki kwa urahisi. Kazi yakiongozi ni kuongoza. Hii haihusu kuwashinda au kuwalazimisha wengine bali inamaanisha “kuwa mbele” kiroho na kutawala. wengine hutambua na kufuata. Neno “ongoza” linapatikana katika 1Tim 5:17 na Waibrania 13: 7, 17, 24 za Bibilia ya King James, labda imekuwa kiini cha wingi wa kutoelewa. Neno hili ni PROISTEMI katika Ugiriki na linafaa kutafsiriwa kumaanisha “kusimama mbele” au “kuongoza.” Mzigo wa kiongozi wa kweli sio katika “ kumiliki kanisa” bali ni kusaidia wengine katika kutimiza huduma zao – wakikua kuwa wale ambao Mungu amewaita wawe. Unaweza kuwatambua kwa urahisi viongozi mahususi kwa vile watazingatia kuhakikisha kukua kiroho na mahitaji ya wengine wameyaweka mbele ya yao.

Viongozi ambao kwa kawaida hujilisha tu (wakijenga huduma zao wenyewe, kukuza hali zao za kifedha, na kadhalika) na kwa sababu hizi kuwanyamazisha wale wanaowatunza, wote watakuwa chini ya hukumu ya Mungu. Wanaojiinua na kuwaacha wenzao wakididimia kwa hisani ya usalama wao, uwezo au mengine wanayoyazingatia, wako katika hali ya kutisha zaidi. (Yakobo 3:1). Uongozi ni lazima uinuliwe na Mungu. Uongozi ukiwa ni kutokana na masomo, kuteuliwa katika cheo, au nia za kibinafsi, bila shaka utazuia kukua kiroho kushirikiana kidini kusikofaa kunaweza kuwa kizuizi katika kutimiza mapenzi ya Mungu.

Kuhakikisha kuwa kazi imefanywa au kuwahusisha watu hakuhakikishi kukomaa kiroho. Bila shaka wasioamini pia wanaweza kufaulu katika kushirikiana. Kazi iliyopo si kuwa na majumba kuu kuu, huduma “zilizostawi” au watu wengi wakihudhuria. Yote haya yanawezafikiwa bila kutimiza nia yake Baba. Katika mpango wake, mipangilio imewakilishwa na huduma za kikweli za kiroho ambazo amekuza kati yetu. Mipango yake ya usoni yanatokana na uongozi wake na hadhi katika mashirika au za kikazi zimewakilishwa na uwezo wa kikweli wa kiroho tukiwa atakavyo Mungu, watu hawapewi kazi kwa kutokana na kile ambacho wangependa kufanya. Kwa mfano tukihitaji walimu wa watoto kanisani au watumishi tutaulizia wale wa kujitolea. Badala yake, uwezo wa kila mtu hugunduliwa kisha wakahimizwa katika njia hizi.

Kwa hivyo, mikutano ya kikristo unayohudhuria itaharibika kabisa vitu visipofanywa hivi, basi nahisi inanibidi kama rafiki na ndugu yako nikufahamishe kuwa hii siyo kazi ya kiroho. Yaweza kuwa ni ushirika tu wa watu ambao hautimizi nia ya Mungu lakini huandamana na njia kisasa za kikristo. Yaweza kuwa unashiriki na kundi la waumini ambao huwahamasishi au kukupa nafasi ya kukua katika huduma zako. Labda umezoea ile hali ya “Mtumishi mmoja” au kilichopangwa kupita kiasi hadi maisha kutoweka ndani yake. Inaweza kuwa kipaji chako kimetupiliwa, kuharibiwa kudharauliwa au kuzuiwa. Bali hakuna hata mojawapo wa hizi kuwa sababu ya kutosha ya kutofanya chochote. Utakapojitokeza mbele ya mfalme, hakuna atakayekuwa wa kumlalamikia kwa kukosa kwako kufanya kazi yako ya uchungaji.

Kwa vile Mungu amekuwezesha na kukuita, atakuandalia njia ya kuanza kuhudumu. Kwa mfano, unaweza kuomba popote na kwa Wakati wowote unaweza kuwapa wengine bila ya kibali cha kisheria. Unaweza kufundisha na kupatiana mwelekezo kutoka nyumba hadi nyingine ikiwezekana.Mradi unaanza kufanya kazi katika huduma aliyokuita Mungu, milango itafunguka mbele yako na watu watautambua mkono wa Mungu katika maisha yako. Mambo yanaweza kuanza polepole mwanzoni na kuonekana kuwa ndogo na kukosa maana (Zekaria 4:10). Lakini mnavyovitumia kwa imani na hekima vipaji alivyowapa Mungu, vitakua na utakua kiroho pia.

Nia ya Mungu kwetu ni tuwe naye katika ufalme wa makuhani. Sote tu manabii wake (1 Wakorintho 14: 1,31). Na kila mmoja wetu ana huduma ya kukamilisha na kazi za kiroho tunazopaswa kufanya ambazo hakuna yeyote mwingine awezaye fanya jinsi tunavyoweza. Tutakapofika mbele ya Mungu tutaitwa ili tutoe hesabu za kazi zetu (Ufunuo 2: 23). . Hapo, yale tuliyoyafanya yataeleza hali zetu za kikweli za kiroho. Hatutaweza kusema kuwa hatukuona mahitaji, au hatukuwa na uwezo wa kutosha (Mathayo 25: 31 – 46). Mungu huyu mmoja aliyetenda miujiza kwa mitume na manabii, yu ndani ya kila ya mmoja wa watoto wake. Anaweza kufanya zaidi ya tunayomwomba au kudhani, tukiwa tumemtii.

Ninasihi kila mmoja wenu ayachukulie mawazo haya kwa uzito. Zingatia maisha yako na utazame kama kwa kweli wewe u mfanyi kazi wa bidii kwa mfalme wako au wewe u mpita njia wa kuzembea. Je umeweka hatua ya “usalama” kati yako na Mungu na kuwaacha wengine kuubeba mzigo ulio jukumu lako? Je umetoweka kwa sababu ya woga au kulemaa katika utu na kuwaacha wengine kufanya hiyo kazi? Ikiwa hivyo, chukua muda sasa na uombe msamaha mbele ya Mungu. Mpe Mungu maisha yako yote kwa mara nyingine. Kisha anavyokuongoza, kwa heshima fanya naye kazi katika shamba lake la mizabibu.

If you want you can download this pamphlet as a PDF here.

We are always looking to offer books in more languages.


Want to help us by translating or proofreading books?

How to volunteer